Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi, katika kikao cha kumi na moja cha uwasilishaji wa mawazo (idea-generation) kwa ajili ya utekelezaji wa ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, kilichofanyika mahsusi kwa mashauriano ya pamoja ya kundi la walimu wa fani ya tablighi kwa anuani “Hawza kinara, fani za tablighi na uwasilishaji wa ujumbe ulio wazi (Balāgh Mubīn)”, kilichofanyika katika ukumbi wa swala wa jengo la Karīmat Ahlul-Bayt (a.s.), Madrasa ya Ma‘ṣūmiyya, Qom, Iran, baada ya kutoa shukrani kwa Naibu wa Elimu wa Hawza za Kielimu, alisema: ninawashukuru wahusika kwa kuandaa mikutano hii na kamati zake za kitaaluma; kwani matokeo ya vikao hivi yatatumika katika mapitio na michoro ya baadaye.
Mkuu wa Hawza za Kielimu Iran, alieleza: Uongozi wa Hawza katika kipindi hiki umepitia njia iliyojaa mafanikio na changamoto. Njia hii imebuniwa juu ya huduma za wenza wetu na takwimu zilizokusanywa kutoka tafiti za uwanjani, tathmini za udhaifu (diagnosis ya matatizo), pamoja na maoni ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na Marji' wa taqlid.
Aliongeza kuwa: katika miaka ya awali, kwa mujibu wa mawasiliano na mipango katika ngazi ya nchi, takwimu kutoka takribani matawi kumi ya masomo zilikusanywa na hatua kwa hatua zikakamilishwa; takwimu hizi zikawa msingi wa mwelekeo wa baadaye wa Hawza, sambamba na kuendelea kwa shughuli za kila siku na za kawaida za Hawza.
Uandaaji wa “Mfumo wa Hati za Msingi na Kimkakati” kwa mara ya kwanza
Ayatullah A‘rafi, akirejea hatua zilizochukuliwa katika mfumo wa upangaji wa Hawza za Kielimu, alitangaza kuandaliwa kwa “mfumo wa hati za msingi na kimkakati” kwa mara ya kwanza katika historia ya Hawza. Akibainisha kuwa mkusanyiko wa madai ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi uliokusanywa katika zaidi ya nukta 300 na kupangwa kwa makundi, alisema: mambo haya, bila upendeleo na kwa umakini, yaliandaliwa katika kijitabu kinachoonesha ni yapi yametekelezwa, yapi yako katika hatua ya utekelezaji, na yapi yanahitaji ufuatiliaji zaidi.
Aliongeza: benki ya mawazo imeanzishwa, ambamo hata mapendekezo yasiyotekelezeka hukusanywa na kuchambuliwa. Kwa msingi wa takwimu hizi, mkusanyiko wa hati za Hawza uliandaliwa; japokuwa huenda kukawa na mitazamo tofauti kuhusu kiwango cha athari zake, lakini ni msingi wa lazima kwa Hawza.
Mkuu wa Hawza za Kielimu, akitangaza kwamba “kwa mara ya kwanza Hawza imepata mfumo wa hati za msingi na kimkakati”, alifafanua: hati hizi zinajumuisha dira (vision), mkataba/kanuni (charter) na mifumo jumuishi kumi na mitano, ambayo imekuwa msingi wa mipango ya baadaye.
Akitaja kukamilika kwa mpango wa kwanza wa miaka mitano wa uongozi wa Hawza, alisema: mwaka huu ni mwaka wa mwisho wa mpango huo na jalada lake linafungwa. Kwa sasa, mpango wa pili wa miaka mitano unaandaliwa, na kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika, takribani asilimia 50 hadi 60 ya karibu programu elfu moja za awali zimefanikiwa kutekelezwa.
Kubuni ramani ya njia na hati 100 za kimkakati za Hawza za Kielimu
Ayatullah A‘rafi aliendelea kurejelea uandaaji wa “hati mia (100) za kimkakati za Hawza za Kielimu” kama mojawapo ya programu za msingi, na akasema: miaka miwili iliyopita huko Mashhad Iran, katika kipindi cha saa kumi, niliwaeleza misingi ya kifalsafa, nguzo na mielekeo ya mipango na hati hizi kwa takribani wasimamizi na walimu 400 wa Hawza.
Fani za elimu za Hawza zimepanuka kutoka 10–15 hadi zaidi ya fani 100 za utaalamu
Ayatullah A‘rafi, akirejea mradi wa kupanga na kubuni fani za Hawza, alitangaza kukamilika na kupitishwa kwa jumla na mitaala ya takribani fani 150 za utaalamu, pamoja na utekelezaji wa zaidi ya fani 100 za utaalamu katika vituo vya Hawza na mikoani.
Akiashiria kuwa mradi huu, baada ya miaka mingi ya juhudi na kazi za kitaalamu, sasa umefikia hatua ya utekelezaji, aliongeza: miongoni mwa mamia ya fani za utaalamu zilizopendekezwa, zaidi ya fani 400 zilipata idhini ya mwisho, na mchakato wa kubuni muundo wa mti wa fani na mada (silabasi) ulianza upya kutoka msingi.
Mkuu wa Hawza za Kielimu, akirejea historia ya mradi huu katika Jāmi‘atul-Mustafā (s) na baadhi ya vituo vingine, alibainisha: kazi hapa ilifanyika kwa uzito zaidi na kwa mtazamo wa kihawza. Leo, jumla ya mitaala ya takribani fani 150 za taaluma zimepitishwa, ambapo kati ya hizo, zaidi ya fani 100 ziko katika utekelezaji. Fani zilizokuwa zinatekelezwa hapo awali zilikuwa takribani 10 hadi 15 tu, lakini sasa zimeongezeka hadi zaidi ya fani 100, na mikoani pia takribani fani 100 zimeanzishwa na kuendeshwa hadi sasa.
Maoni yako